10 ZILIZOVUMA 2024
UDADAVUZI: Fahamu saratani ya shingo ya kizazi
Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au seli zilizoko katika shingo ya kizazi wengine wakiita mlango wa kizazi.
Fahamu kuhusu Kifua Kikuu au TB, kwa nini wengine huugua mara kwa mara?
Kifua Kikuu au (TB) ni ugonjwa wa kuambukiza ambao huathiri mapafu na kusababishwa na bakteria. Ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa wakati watu walioambukizwa wanapokohoa, kupiga chafya au kutema mate.
Fahamu kuhusu ugonjwa wa kifafa kwa mujibu wa WHO
Kifafa ni ugonjwa sugu wa ubongo unaohusisha mtu kupata mshituko katika ubongo na kusababisha degedege au kuanguka kifafa hali ambayo hutofautina ukubwa kulingana na ukubwa wa mshituko.
Fahamu mambo 10 ya kutokomeza ukatili wa kijinsia
Ukatili dhidi ya wanawake na wasichan unasalia kuwa kitendo cha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani kote, ukiathiri zaidi ya wanawake milioni 1.3, takwimu ambayo hata hivyo haijabadilika kwa zaidi ya muongo mmoja.
Mwongozo mpya kuhusu utoaji mimba utanusuru maisha ya wanawake na wasichana:WHO
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limetoa mwongozo mpya kuhusu huduma ya utoaji mimba kwa lengo la kulinda afya ya wanawake na wasichana na kusaidia kuzuia zaidi ya visa milioni 25 vya utoaji mimba usio salama ambao hivi sasa unafanyika kila mwaka.
Sababu 6 kwa nini wanawake wana njaa zaidi kuliko wanaume
Februari 20 ni maadhimisho ya siku ya haki ya masuala ya kijamii. Lakini tunaendelea na muongo mpya tukiwa na chini ya miaka 10 kufikia lengo la kuwepo usawa wa kijinsia. Kwa bahati mbaya bado tuna safari ndefu kwa kitu kilicho muhimu kama chakula na takribani theluthi mbili ya nchi zote duniani wanawake wako kwenye hatari zaidi ya kufa njaa. Kwa kila suala linalowabagua wanawake hufuata lingine la kuwaweka wanawake karibu na umaskini na njaa.
Harakati za kuelimisha umma kuhusu Usonji
Ugonjwa wa Usonji kwa kiingereza Autism, ni ugonjwa ambao kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO hukumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani. Usonji ni tatizo la kibaiolojia analopata mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake na dalili huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea.