Kilimo kwenye mstari wa mbele katika hatua za dharura DRC
Sasa, wanaishi hapa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rusayo 2 ili kuepuka mzozo unaoendelea katika eneo hilo na kujilinda wao na watoto wao, wakitumai siku moja kuanza maisha mapya.
Content-Length: 158219 | pFad | http://news.un.org/sw/news/topic/migrants-and-refugees
Sasa, wanaishi hapa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rusayo 2 ili kuepuka mzozo unaoendelea katika eneo hilo na kujilinda wao na watoto wao, wakitumai siku moja kuanza maisha mapya.
"Wasyria wanastahili kupata kile wanachotarajia wakirejea nyumbani, kama vile usalama, misaada na utulivu,” amesema Amy Pope, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi baada ya kumaliza ziara yake katika taifa hilo la Mashariki ya Kati.
Kutana na Saido Omar Noor, binti mwenye umri wa miaka 25 mkimbizi kutoka Somalia anayeishi Kakuma kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Kenya. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema katika jamii yake ni yeye mwanamke pekee wa Kisomali anayecheza mpira kwa kikapu au basketball.
Makumi ya raia wakiwemo wanawake, wanaume na watoto wanaokimbia vita nchini Sudan na Kwenda kusaka usalama nchini Uganda wamewasimulia wataalam wa haki za binadamu jinamizi walilopitia.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na wadau mbalimbali wa haki za binadamu imetoa wito kwa mataifa yote kuwalinda wakimbizi na wahamiaji walio katika hatari baharini, ikiwa ni pamoja na kupitia operesheni zilizoimarishwa za utafutaji na uokoaji SAR, na kwa kuhakikisha kuwa waokoaji hawachukuliwi kama wahalifu.
Usafirishaji haramu wa wahamiaji ni uhalifu unaofanywa ili kupata faida, unaoendeshwa na hitaji la kuvuka mipaka nje ya njia za kawaida na kuathiri nchi nyingi kote kote duniani.
Nimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi.
Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.
Kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia Chad wakitoka Sudan kuwa ni wanawake na watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA limeimarisha huduma za afya ya wanawake na watoto.
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11 amenusurika kifo na kuokolewa kwenye boti iiyozama Lampedusa mwambao wa Italia huku abiria wengine wote 44 waliokuwa kwenye boti hiyo wakiwemo wanawake na watoto wakiaminika kuzama kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataiifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Fetched URL: http://news.un.org/sw/news/topic/migrants-and-refugees
Alternative Proxies: