Content-Length: 172861 | pFad | http://news.un.org/sw/audio-product/makala

Makala | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNHCR

Wasichana wakipewa fursa hakuna mchezo utakaowashinda: Saido Noor

Kutana na Saido Omar Noor, binti mwenye umri wa miaka 25 mkimbizi kutoka Somalia anayeishi Kakuma kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Kenya. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema katika jamii yake ni yeye mwanamke pekee wa Kisomali anayecheza mpira kwa kikapu au basketball. Flora Nducha na taarifa zaidi..

Sauti
3'31"
FAO Tanzania

FAO Tanzania yatoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa wenyeji Tanzania kupitia Mradi wa ACP MEAs 3

Mradi wa ACP MEAs 3 unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, na kufadhiliwa na Muungano wa Ulaya, EU umetoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wakulima nchini Tanzania. Mradi huu unawapa wakulima zana na ujuzi muhimu katika ufugaji nyuki endelevu, na hivyo kuboresha maisha yao huku wakikuza bayoanuwai na uhifadhi wa mazingira. Kwa kuunga mkono jamii za wenyeji, Mradi huu unalenga kukuza ukuaji wa uchumi na kuwawezesha wakulima kulinda wachavushaji, ambao ni muhimu kwa uzalishaji katika kilimo na afya ya mfumo ikolojia.

Sauti
2'50"
UNICEF

Harakati za wazazi kuona watoto wao wanasajiliwa nchini mwao baada ya kuzaliwa

Tarehe 11 mwezi huu wa Desemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilitoa ripoti yake kuhusu usajili wa vizazi duniani ikionesha maendeleo makubwa katika idadi ya watoto wanaosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Maeneo mengine kama nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ongezeko ni dogo ikilinganishwa na kwingineko. Ingawa hivyo licha ya changamoto zilizoko kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara katika kutoa huduma hiyo, mafanikio yanaanza kuonekana kama inavyosimulia makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi kupitia video ya UNICEF.

Sauti
4'24"
FAO/Tanzania

Sasa tunalima mboga shuleni na nyumbani - Wanafunzi Buhigwe Tanzania

Kupitia mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP,  awamu ya Pili, Shule ya Msingi Buhigwe, iliyoko wilayani Buhigwe, mkoa wa Kigoma, ilipatiwa mafunzo kupitia Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), likishirikiana na asasi isiyo ya kiserikali RECODA. Mafunzo haya yalilenga mbinu bora za kilimo ambapo wanafunzi waliweza kuanzisha bustani za mboga kupitia somo la Elimu ya Kujitegemea. Mradi umeanza kutekelezwa na matunda yanaanza kuonekana kama asimuliavyo Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Sauti
3'42"
MONUSCO/Abel Kavanagh

Simfahamu baba yangu, natamani nimfahamu kwani nakosa upendo wake

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanazuiwa kutumia chakula, fedha au vitu vingine kwa ajili ya kushawishi ngono kutoka kwa mtu mwingine. Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zinachukua hatua zaidi kuepusha ukosefu huo wa maadili , lakini bado visa hivyo vinaendelea kutokea. Katika baadhi ya matukio, watoto waliozaliwa kupitia uhusiano wa aiana hiyo wanasalia nyuma kwenye mazingira ya mizozo ambako baada ya baba zao kumaliza kuhudimia, huondoka na kubaki bila baba.

Sauti
3'49"
© WFP/Lisa Murray

Asante WFP kwa kusambaza dawa za kuua magugu mmebadii maisha yangu: Mkulima Catherine Wanjala

Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP wa kusambaza dawa ya bioherbicide ya kuuwa magugu kwenye mashamba ya mtama na mahindi kwa wakulima wa Kakamega magharibi mwa Kenya umekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima kama Catherine Wanjala ambaye  magugu hayo yalimuharibia mazao na hata kuilazimisha familia yale  kulala njaa wakati  mwingine kwa kukosa chakula. Kwaa ufafanuzi zaidi ungana na Flora Nducha katika makala hii.

Sauti
3'35"
IFAD

Mradi wa IFAD wasaidia vijana Senegal kusalia nchini mwao, kulikoni?

Mradi wa uitwao Agri-Jeunes uliozinduliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD ili kusaidia raia wa Senegal kuondokana na umaskini, na janga la njaa, umewapatia vijana wa kiume na wa kike matumaini ya kusalia nchini mwao badala ya kuhamia ughaibuni. Mradi huu umewasaidia vijana hao kwa mafunzo ya kilimo, ufugaji kuku, uvuvi na stadi za kuendesha biashara ndogondogo.

Sauti
4'7"








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/audio-product/makala

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy