Simulizi ya mama aliyebakwa yeye na watoto wake DRC na ombi lao kwa UN
Majambazi waliingia nyumbani wakatubaka nakuchukua vitu vyote pia akanitoboa hadi leo mwili umeharibika, ni kauli ya Chantale, jina lake halisi linahifadhiwa kwa usalama wake, na ni miongoni mwa manusura wa ukatili wa kingono katika mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.