Content-Length: 166367 | pFad | http://news.un.org/sw/news/topic/sdgs

Malengo ya Maendeleo Endelevu | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana Cox’s Bazaar nchini Bangladesh.
ILO

Sikufahamu ufundi bomba ni nini, sasa ILO imeniwezesha – Msichana Bangladesh

Nchini Bangladesh, mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana kuvunja mwiko na kuingia kwenye tasnia ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume, mathalani ufundi bomba. Mradi huo unaolenga wanufaika 24,000 wenye umri kati ya miaka 18 na 35 unatekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh.

Sauti
1'40"
Mwanafunzi nchini Viet Nam akitoa mbegu
© UNICEF/Truong Viet Hung

Janga la tabianchi: mambo 5 ya kuzingatia 2025

Mji wa Amazon wa Belém, Brazili, utakuwa kitovu cha juhudi za kimataifa za kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi mwezi Novemba 2025, wakati utakapoandaa moja ya mikutano muhimu ya Umoja wa Mataifa ya mabadiliko ya tabianchi hivi karibuni.

Watu wakiwa ufukweni kujipooza na joto kali baada ya tahadhari kutolewa kuhusu joto la kupindukia katika miji kadhaa barani Ulaya 2023 (Kutoka Makataba)
© Unsplash/Domenico Daniele

Mwaka 2024 kuvunja rekodi ya joto kali: WMO

Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hew diniani WMO, limesema mwaka 2024 unatarajiwa kuvunja rekodi ya kuwa mwaka wa joto kali zaidi ukiwakilisha muongo wa joto ambalo halijawahi kushuhudiwa linalochochewa na shughuli za binadamu.

Alaa Khattab (kushoto) kijana aliyekuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara wa kilimo nchini Syria.
FAO

Kutoka kuwa mzalishaji mdogo kijijini kwake hadi kuwa msafirishaji wa Kikanda wa achari: Hadithi ya Alaa Khattab

Mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO ujulikanao kama Nabta kwa lugha ya Kiarabu ukimaanisha "mche" ambao lengo lake ni kuwasaidia vijana wajasiriamali kubadili mawazo yao kuwa  biashara ya kilimo yenye mafanikio umeleta nuru kwa Alaa Khattab kijana aliyekuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara wa kilimo nchini Syria. 

Sauti
2'9"
Mradi wa  umwagiliaji warejesha matumaini kwa wakulima wa Masvingo, Zimbabwe.
IFAD

Mradi wa  umwagiliaji warejesha matumaini kwa wakulima wa Masvingo, Zimbabwe

Hivi karibuni mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia kuzuia kuenea kwa jangwa, ulikunja jamvi huko Riyadh, Saudi Arabia ambapo Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD ulitumia fursa hiyo kuelezea harakati zake za kusaidia wakulima barani Afrika walioathiriwa vibaya na kuenea kwa jangwa. Miongoni mwa mataifa hayo ni Zimbabwe ambako IFAD imeshaanza kuchukua hatua na kuleta nuru kwa wakulima.

Sauti
3'9"








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/news/topic/sdgs

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy