Content-Length: 161015 | pFad | http://news.un.org/sw/news/topic/un-affairs

Masuala ya UM | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Masuala ya UM

Harakati za wazazi kuona watoto wao wanasajiliwa baada ya kuzaliwa.
UNICEF

Harakati za wazazi kuona watoto wao wanasajiliwa baada ya kuzaliwa

Tarehe 11 mwezi huu waDesemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilitoa ripoti yake kuhusu usajili wa vizazi duniani ikionesha maendeleo makubwa katika idadi ya watoto wanaosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Maeneo mengine kama nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ongezeko ni dogo ikilinganishwa na kwingineko. Ingawa hivyo licha ya changamoto zilizoko kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara katika kutoa huduma hiyo, mafanikio yanaanza kuonekana.

Sauti
4'24"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia mkutano wa G20 mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
United Nations

2025 uwe ni mwaka wa Afrika kupata haki zake - Guterres

Mwaka 2025 ni lazima uwe mwaka wa kuhakikisha bara la Afrika linapata haki yake, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini Pretoria, nchini Afrika Kusini hii leo, kwenye ziara ambayo amesema ni ya kuonesha mshikamano na pia kusaka haki, wakati huu ambapo taifa hilo limechukua Urais wa kundi la nchi 20, G20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

Mnara wa urefu wa futi 30 uliopatiwa jina "Funga bomba la plastiki" ulioandaliwa na msanii na mwanaharakati kutoka Canada Benjamin Von Wong ukiwe nje ya eneo ambako kulifanyika Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa huko Nairobi, Kenya.
UNEP/Cyril Villemain

Tuna fursa ya kihistoria ya kujenga ulimwengu usio na uchafuzi wa plastiki - Guterres

Mmekusanyika ili kukamilisha mkataba wa kihistoria wa kukomesha uchafuzi unaotokana na plastiki - hatua muhimu ya kulinda sayari yetu, ndivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alivyoianza hotuba yake kwa njia ya video kwa wajumbe kutoka nchi 175 walikusanyika katika jiji la Busan nchini Korea Kusini, Jumatatu hii ya Novemba 25 kwa ajili ya mkutano wa tano wenye lengo la kupata mkataba wa kimataifa wa kuzuia uchafuzi unaotokana na plastiki.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/news/topic/un-affairs

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy