Utamaduni wa Kiswahili umeniinua kiuchumi: Namayombo Mgonela
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa.
Content-Length: 158939 | pFad | http://news.un.org/sw/news/region/americas
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa.
Idadi ya watoto wanaoandikishwa katika makundi yenye silaha nchini Haiti imeongezeka kwa asilimia 70 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.
Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.
Jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia imevumilia miongo kadhaa ya migogoro na watu kutawanywa inayosababishwa sio tu na mabadiliko ya tabianchi mila kandamizi bali pia kupotea kwa viumbe hai na hivyo kutishia maisha yao.
Kufuatia Donald J. Trumpov kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Jumanne Novemba 5, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa salamu za pongezi.
Nchi tofauti kutoka kote ulimwenguni zimekusanyika katika jiji la Cali, Colombia,kujadili jinsi ya kulinda bayoanuwai na kuunda mpango wa kudumu wa jinsi binadamu wanavyoweza kuishi kwa amani na asili.
Mabadiliko ya tabianchi yanapoendela kujadiliwa nchini Colombia, aina ya maharagwe yenye ladha nzuri na stahimilivu ambayo imekuwepo kwa karne nyingi inaweza kuwa jawabu kwa watu wa jamii ya asili ya Wayúu nchini Colombia.
Hali ya kibinadamu nchini Haiti inazidi kuwa mbaya huku mamilioni ya watu wakikabiliwa na ukosefu wa chakula, huduma za afya, na elimu. Ghasia zinazotokana na makundi ya wahalifu zimekuwa kikwazo kikubwa kwa jitihada za kutoa msaada. Hapa tunachambua mambo sita yanayodhihirisha ukubwa wa janga hili na hatua zinazochukuliwa kukabiliana nalo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), linatoa mwito wa kuongezwa na kushughulikiwa kwa haraka, uungwaji mkono na utatuzi kwa Wahaiti walioathiriwa na ghasia na ukosefu wa usalama, wakiwemo wale waliofurushwa kwa nguvu, imeeleza taarifa ya shirika hilo iliyotolewa leo Oktoba 4 jijini Geneva, Uswisi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeripoti kuwa zaidi ya watu 700,000, nusu yao wakiwa watoto, wamekimbia makazi yao ndani ya Haiti kufuatia kuongezeka kwa machafuko. Ripoti hiyo mpya inaonesha ongezeko la asilimia 22 la wakimbizi wa ndani tangu mwezi Juni, huku hali ya kibinadamu nchini humo ikiendelea kuzorota.
Fetched URL: http://news.un.org/sw/news/region/americas
Alternative Proxies: