Asante MONUSCO kwa kutuwezesha kiuchumi mwaka 2024 – Wanawake Beni DRC
Ufadhili uliofanikishwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC (MONUSCO) umeniinua kiuchumi na kunipatia matumaini mwaka huu wa 2024 kwani nimewezakuendelea na biashara yangu, amesema Elena Claudine mama Josée, Mfanyabiashara kwenye soko la Mayangose.