Guterres alaani mauaji ya watumishi wa WFP nchini Sudan
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amechukizwa na taarifa za mauaji ya wafanyakazi watatu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP nchini Sudan.
Content-Length: 156501 | pFad | http://news.un.org/sw/news/topic/humanitarian-aid
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amechukizwa na taarifa za mauaji ya wafanyakazi watatu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP nchini Sudan.
"Wasyria wanastahili kupata kile wanachotarajia wakirejea nyumbani, kama vile usalama, misaada na utulivu,” amesema Amy Pope, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi baada ya kumaliza ziara yake katika taifa hilo la Mashariki ya Kati.
Siku kumi na moja tangu kukoma kwa utawala wa kiimla uliodumu kwa miongo mitano nchini Syria, viongozi wa ngazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa wamendelea kusisitiza hitaji la kutanguliza ulinzi wa manusura na uhifadhi wa ushahidi wa uhalifu.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na wadau mbalimbali wa haki za binadamu imetoa wito kwa mataifa yote kuwalinda wakimbizi na wahamiaji walio katika hatari baharini, ikiwa ni pamoja na kupitia operesheni zilizoimarishwa za utafutaji na uokoaji SAR, na kwa kuhakikisha kuwa waokoaji hawachukuliwi kama wahalifu.
Katika harakati za kurejesha huduma za afya nchini Syria baada ya miaka 14 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosambaratisha huduma hizo kwa wananchi, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP limefikisha nishati ya mafuta kwenye hospitali ya Zahi Azraq mjini Aleppo kaskazini mwa nchi.
Takriban watu milioni moja wa Gaza wanakabiliwa na hatari ya kuishi majira ya baridi bila makazi ya kutosha huku mashirika ya Umoja wa Mataifa yakihaha kutoa msaada wa kukabiliana na hali ya hewa ya baridi, wakati kukiwa na mashambulizi yanayoendelea ya Israel, maagizo ya mara kwa mara ya watu kuhama na vikwazo vya kuwasilisha misaada, yameonya leo mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.
Siku 11 baada ya kuanguka kwa utawala wa Assad nchini Syria, wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamejulishwa kuwa wasyria hivi sasa licha ya matumaini bado wamegubikwa na hofu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema limeshafikisha msaada wa chakula kwa watu 800,000 wanaokabiliwa na baa la njaa na walio katika hatari ya baa la njaa katika maeneo mbalimbali nchini Sudan tangu ilipozindua kampeni kubwa ya kusambaza msaada wa chakula katika taifa hilo lililoghubikwa na vita iliyozuka upya Aprili 2023.
Wakati ripoti ya hivi karibuni ya shirika la Umoja wa Mataifa ikisema na ukimwi UNAIDS kuna mafanikio makubwa yamepatikana katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU ambayo yamepungua kwa asilimia 39 tangu 2010 duniani kote, na kwa asilimia 59 mashariki na kusini mwa Afrika, bado wagonjwa wapya wanapatikana hususani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwa ni pamoja na Uganda, ripoti kutoka kwa kamisheni ya Ukimwi ya nchi hiyo (UAC) inasema kuna watu milioni 1.4 wanaishi na virusi vya ukimiwi au VVU nchini humo, na vijana ni asilimia kubwa.
Tarehe 11 mwezi huu waDesemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilitoa ripoti yake kuhusu usajili wa vizazi duniani ikionesha maendeleo makubwa katika idadi ya watoto wanaosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Maeneo mengine kama nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ongezeko ni dogo ikilinganishwa na kwingineko. Ingawa hivyo licha ya changamoto zilizoko kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara katika kutoa huduma hiyo, mafanikio yanaanza kuonekana.
Fetched URL: http://news.un.org/sw/news/topic/humanitarian-aid
Alternative Proxies: