Content-Length: 160430 | pFad | http://news.un.org/sw/features

Makala Maalum | 1 Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Mzozo nchini Syria umesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao. (Maktaba)
© WFP

Kusaka amani Syria: Fursa kubwa, hatari kubwa

Kufuatia kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad nchini Syria, Jumapili ya tarehe 8 mwezi Desemba 2024, Syria imeingia katika kipindi cha sinfofahamu, na Umoja wa Mataifa utakuwa na dhima muhimu ya kuhakikisha mpito tulivu utakaosongesha hatua za kurekebisha taasisi, kuzifanya ziwe tulivu. Halikadhalika kuendeleza juhudi za kuleta pamoja makundi na pande mbalimbali ambayo yaliibuka baada ya kuanza kwa vita mwaka 2011.

Siddhesh Sakore (kulia) anafanya kazi na wakulima huko Pune, India.
UNCCD

Kutana na mashujaa wa ardhi wanaopambana na kuenea kwa jangwa duniani: UNCCD

Kuanzia kupanda miti bilioni moja nchini Zimbabwe, kusini mwa Afrika, hadi kusafirisha bidhaa kutoka kwenye mti wa moringa nchini Mali na kuanzisha mchezo wa bodi unaozingatia mbadiliko y tabianchi unaoitwa "Kuokoa Penguin," nchini Costa Rica, kundi la vijana kimetambuliwa na Umoja wa Mataifa kwa kuleta matokeo chanya katika mapambano ya kukabiliana na kuenea kwa jangwa, uharibifu wa ardhi na ukame.

Wanawake na wanaume huko Samburu Kenya wakishiriki katika mafunzo ya usimamizi wa ardhi yaliyowezeshwa na FAO.
FAO/Kenya

Jinsi usawa wa kijinsia katika umiliki wa ardhi unavyochochea ukulima na uhakika wa chakula Kenya

Mpango wa Usimamizi wa Ardhi uliopatiwa jina "Kusaidia kufikia Ajenda 2030 kupitia mageuzi chanya ya ugatuzi wa ardhi katika maeneo ya ardhi za jamii nchini Kenya" umeboresha uhakika wa kupatikana kwa chakula na lishe kupitia upatikanaji wa ardhi kwa wote nchini Kenya. Programu hii imezinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya (EU) katika kaunti 9 ikilenga kuimarisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi.

Sauti
5'5"
Dkt. Philip Awezaye mhadhiri wa chuo kikuu cha KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini.
UN News/Flora Nducha

Waafrika hata siri hatuna sababu ya lugha za kigeni, lazima tuwe na lugha yetu: Dkt. Awezaye

Huko Havana Cuba Kongamano la kimataifa la Kiswahili limekunja jamvi mwishoni mwa wiki ambapo wadau kutoka nchi mbalimbali kuanzia barani Ulaya, Marekani kaskazini na Kusini, Asia na wenyeji Afrika walikutana na kujadili jinsi ya kukuza lugha ya Kiswahili duniani sanjari na kutekeleza malengo ya Umoja wa Mataifa kama kutumia Kiswahili kudumisha amani na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/features

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy