Content-Length: 97603 | pFad | http://news.un.org/sw/story/2020/01/1078651

UNHCR yatunukiwa kombe la IOC kwa huduma kwa wakimbizi kupitia michezo | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatunukiwa kombe la IOC kwa huduma kwa wakimbizi kupitia michezo

Rais wa IOC, Thomas Bach akimtunuku Kamishina Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi kombe la Olimpiki
IOC/Christophe Moratal
Rais wa IOC, Thomas Bach akimtunuku Kamishina Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi kombe la Olimpiki

UNHCR yatunukiwa kombe la IOC kwa huduma kwa wakimbizi kupitia michezo

Wahamiaji na Wakimbizi

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC leo imelitunukia tuzo ya juu ya kikombe cha  Olimpiki shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR kwa sababu ya kazi zake za kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadhi kupitia michezo na kuchagiza maadili ya Olimpiki kote duniani.

Kikombe cha Olimpiki kilianzishwa mwaka 1906 na Pierre de Coubertin mwanzilishi wa IOC na kinatolewa kila mwaka kwa shirika ambalo linatoa huduma ya kipekee kupitia michezo au kuchagiza maadili ya Olimpiki.

Akipokea tuzo hiyo Kamishina Mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi amesema “tuzo hii heshima ninayotaka kushirikiana na wafanyakazi wenzangu wote kote duniani ambao wamefanya Zaidi ya wanayopaswa kuleta fursa kwa watu waliotawanywa kote duniani kupitia michezo, hata katika mazingira ambayo ni changamoto kubwa. Na bila shaka tuzo hii pia ni kwa wat una jamii zilizotawanywa ambazo zinahudumiwa na UNHCR, ambazo zinaelewa uwezo wa michezo kuleta mabadiliko na kutumia fursa hizo ambazo wamepewa.”

Kwa upande wake Rais wa IOC Thomas Bach akikabidhi tuzo hiyo amesema “UNHCR amekuwa mdau mkubwa wa kuchagiza maadili ya IOC. Dhamira ya IOC na timu nzima ya Olimpiki kusaidia wakimbizi inatokana na msingi wa Imani yetu katika uwezo wa michezo kuifanya dunia kuwa mahala bora pa kuishi.”









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/story/2020/01/1078651

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy