Content-Length: 99433 | pFad | http://news.un.org/sw/story/2024/10/1181541

Baraza la Usalama lajadili uwezekano wa vikosi vya Korea Kaskazini kuisaidia Urusi dhidi ya Ukraine | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili uwezekano wa vikosi vya Korea Kaskazini kuisaidia Urusi dhidi ya Ukraine

Miroslav Jenča, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Ulaya, Asia ya Kati na Amerika katika Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Siasa na Ujenzi wa Amani na Operesheni za Amani, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu vitisho kwa amani na usalama…
UN Photo/Manuel Elías
Miroslav Jenča, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Ulaya, Asia ya Kati na Amerika katika Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Siasa na Ujenzi wa Amani na Operesheni za Amani, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu vitisho kwa amani na usalama wa kimataifa.

Baraza la Usalama lajadili uwezekano wa vikosi vya Korea Kaskazini kuisaidia Urusi dhidi ya Ukraine

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa una wasiwasi kuhusu taarifa za kikosi cha kijeshi cha Korea Kaskazini kutumwa Urusi na uwezekano wake wa kupelekwa katika eneo la migogoro, Miroslav Jenca, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Ulaya, Asia ya Kati na Amerika, amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo Jumatano Oktoba 30.

Kikao hicho cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu uwezekano wa kuhusika kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini katika mzozo huo kimeombwa na Ukraine ambayo imeungwa mkono na nchi kadhaa ikiwemo Korea Kusini.
 
"Umoja wa Mataifa hauna maelezo zaidi kuhusu suala hili na hauko katika uwezo wa kuthibitisha madai au ripoti zilizopokelewa," amesema na kuongeza, "ufahamu wetu kuhusu suala hili kwa hivyo unategemea tu habari ambayo iko mitandaoni."
 
Makadirio ya idadi ya askari 'yanatofautiana sana'
 
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari na taarifa za maafisa wa nchi wanachama, Jenca ameendelea, askari kutoka DPRK wamewasili Urusi. "Makadirio ya idadi yao yanatofautiana sana," ameongeza.
 
Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa amekumbushia kuwa mnamo Juni 19, 2024, "Mkataba wa Ushirikiano wa Kimkakati kati ya Shirikisho la Urusi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea" ulitiwa saini huko Pyongyang. Hati hii, msemaji inatoa ushirikiano katika masuala yanayohusiana na usalama na ulinzi.
 
Kuidhinishwa kwa mkataba wa kijeshi na DPRK
 
Mkataba huo, Jenca amefahamisha wanachama wa Baraza la Usalama, uliidhinishwa na baraza la chini la bunge la Urusi, Jimbo la Duma, mnamo Oktoba 24. "Inatarajiwa kwamba baraza la juu pia litaunga mkono," amebainisha.
 
Pia amekumbushia kwamba kulikuwa na ripoti za awali kwamba DPRK imesafirisha makombora ya angani na makombora ya mizinga hadi Urusi "kwa matumizi iwezekanavyo katika operesheni zake za kijeshi nchini Ukraine."
 
 








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/story/2024/10/1181541

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy