Content-Length: 108006 | pFad | http://news.un.org/sw/story/2024/12/1182801

Kutana na mashujaa wa ardhi wanaopambana na kuenea kwa jangwa duniani: UNCCD | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutana na mashujaa wa ardhi wanaopambana na kuenea kwa jangwa duniani: UNCCD

Siddhesh Sakore (kulia) anafanya kazi na wakulima huko Pune, India.
UNCCD
Siddhesh Sakore (kulia) anafanya kazi na wakulima huko Pune, India.

Kutana na mashujaa wa ardhi wanaopambana na kuenea kwa jangwa duniani: UNCCD

Tabianchi na mazingira

Kuanzia kupanda miti bilioni moja nchini Zimbabwe, kusini mwa Afrika, hadi kusafirisha bidhaa kutoka kwenye mti wa moringa nchini Mali na kuanzisha mchezo wa bodi unaozingatia mbadiliko y tabianchi unaoitwa "Kuokoa Penguin," nchini Costa Rica, kundi la vijana kimetambuliwa na Umoja wa Mataifa kwa kuleta matokeo chanya katika mapambano ya kukabiliana na kuenea kwa jangwa, uharibifu wa ardhi na ukame.

Mashujaa Kumi kutoka kote ulimwenguni, wote wako chini ya umri wa miaka 35, wamechaguliwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa UNCCD kushirikisha mafanikio na mawazo yao ya usimamizi endelevu wa ardhi katika kukabiliana na tishio linaloongezeka la kuenea kwa jangwa duniani na upotevu wa ardhi.

Wakati mkutano wa 16 wa kimataifa wa UNCCD kuhusu kuenea kwa jangwa, au COP16, ukiendelea Riyadh, kukutana na Mashujaa hao wa Ardhi wa 2024 na kusoma jinsi wanavyoweza kuhamasisha mabadiliko, kuunganisha wenzao, kutoa ushauri na kuonyesha nguvu ya mageuzi ya hatua za pamoja.

Rokiatou Traoré kutoka Mali

Rokiatou Traoré anajielezea kama "mjasiriamalianayejali mazingira " na amekuwa akifanya kazi nchini Mali kukuza biashara ya kijamii inayotokana na bidhaa kutoka kwenye mti wa moringa.

Rokiatou Traoré akionesha mche wa mzunze.
UNCCD
Rokiatou Traoré akionesha mche wa mzunze.

Takriban wanawake 100 wamefunzwa kutengeneza bidhaa kutoka kwenye miti 20,000. Bidhaa hizo ni pamoja na chai ya asili, poda, mafuta, sabuni, viungo, na vyakula vya watoto ambavyo vimesafirishwa kwa zaidi ya nchi saba.

Mwaka 2023, alizalisha vitalu 150,000 vya mti wa moringa vinayostahimili ukame kwa ajili ya wanawake 5,000 na wakulima vijana.

"Mbegu ni maisha katika usingizi” anasema. "Ipe maji, udongo na ulinzi na inaweza kukabiliana na kuenea kwa jangwa, umaskini wa wanawake na utapiamlo kwa manufaa ya jamii. "

Mipango yake ya baadaye ni kabambe. Ifikapo mwaka 2030, anataka kuanzisha mtandao wa mamilioni ya wanawake wazalishaji wa moringa, kupanda miti milioni 10 ya Moringa na kuuza nje bidhaa za moringa katika masoko ya kitaifa, kikanda na kimataifa kwani anaamini "Hakuna lisilowezekana kufanikiwa penye nia isiyoyumba."

Takudzwa Ashley Mlambo kutoka Zimbabwe

Kupanda miti pia ni ajenda kuu ya Takudzwa Ashley Mlambo kwani ni muhimu kwa juhudi za kuzalisha upya ardhi na kubadili hali ya jangwa.

Takudzwa Ashley Mlambo (kulia) akizungumza na vijana katika bustani moja nchini Zimbabwe
UNCCD
Takudzwa Ashley Mlambo (kulia) akizungumza na vijana katika bustani moja nchini Zimbabwe

Shirika lake linaloongozwa na vijana la Forestry & Citrus Research (FACIR), linalenga kupanda na kufuatilia jumla ya miti bilioni moja nchini Zimbabwe.

Kama mvumbuzi msumbufu anayejikiri mwenyewe, anatumia akili mnemba na ufuatiliaji wa satelaiti ili kusimamia mpango huo.

Anatambua kuwa upandaji miti upya ni hatua muhimu ya kuchukua ili kupunguza kasi ya mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha viwango vya joto duniani kuwa chini ya nyuzi joto 1.5 juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa maendeleo ya viwanda.

Anasema "Tunahitaji kujikita na kijani kibichi zaidi, kadiri inavyokuwa hali ya baridi."

Billie Crystal G. Dumaliang- Ufilipino

Ufilipino ni moja ya nchi zinazoshambuliwa zaidi duniani na hatari za majanga ya asili na hatari hizi ni kama vile vimbunga vilivyoikumba nchi hiyo hivi karibuni na vinazidi kuwa vikali kutokana na mermaidlike ya tabianchi.

Billie Crystal G. Dumaliang amejitolea katika upandaji miti upya.
UNCCD
Billie Crystal G. Dumaliang amejitolea katika upandaji miti upya.

Ukataji miti katika ardhi na maeneo ya maji karibu na mji mkuu wa Ufilipino, Manila, umeweka jiji hilo katika hatari kubwa ya hali mbaya ya mabadiliko ya tabianchi.

Billie Crystal G. Dumaliang na Wakfu wa Masungi Georeserve anaoongoza wamejitolea katika mpango kabambe wa upandaji miti upya unaolenga kurejesha takriban ekari 2,700 za maeneo ya vyanzo vya maji yaliyoharibiwa yanayozunguka Georeserve.

Mradi huo ni muhimu kwa kuimarisha ulinzi wa asili wa Katikati yam ji wa Manila dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

"Wafilipino wanakabiliwa na athari mbaya za ukame na uharibifu wa ardhi kwa kilimo, ustawi, na maisha ya kila siku," amesema, "hivyo tunahitaji kuhifadhi bioanuwai na kupunguza athari za ukame na mabadiliko ya tabianchi.”

Shirika langu hufanya hivi kupitia ulinzi wa ardhi, upandaji miti upya, na simulizi za hadithi zenye matokeo Chanya vinaoendeshwa na utalii endelevu wa kijiografia.

Siddhesh Sakore kutoka India

Akiwa amekulia katika kile ambacho kimeelezwa kuwa "familia ya wakulima iliyotengwa", Siddhesh Sakore amejionea mwenyewe matatizo ya kiuchumi ambayo wakulima na familia zao wanavumilia.

Siddhesh Sakore akitunza mimea katika shamba huko Pune, India
UNCCD
Siddhesh Sakore akitunza mimea katika shamba huko Pune, India

Moja ya masuala muhimu ambayo shirika lake la AGRO RANGERS limezingatia ni uharibifu wa udongo, ambao huathiri moja kwa moja uzalishaji wa ardhi na hivyo maisha ya wakulima.

Uharibifu wa udongo unaweza kusababishwa na matumizi yasiyofaa au usimamizi mbaya pamoja na mmomonyoko, mafuriko, jangwa na kuchafuliwa na kemikali.

Ndoto yake ni kutengeneza riziki kwa wakulima, haswa katika maeneo yenye ukame ya Pune ambako anafanya kazi kwa mhamo kutoka kwenye kilimo cha kemikali hadi kilimo cha miti-hai.

"Katika AGRO RANGERS, tunaamini kuwa vita dhidi ya kuenea kwa jangwa na ukame wa ardhi huanza na mbinu endelevu za kilimo zinazoendeshwa na jamii na mbinu bunifu za kilimo mseto."

Ameongeza kuwa "Kwa kuwawezesha wakulima na maarifa na zana za kujumuisha miti na mazao katika mifumo yao ya kilimo, tunarejesha na kulinda udongo, na kutunza ardhi kwa mustakabali thabiti na endelevu."

Astrid Peraza kutoka Costa Rica

"Kufanya kazi peke yako sio chaguo la kuleta mabadiliko ya maana," amesema Astrid Peraza akiongeza kuwa kwa hivyo amejaribu maoni haya kama mwalimu wa tabianchi kwa vijana huko Costa Rica kwa kuunda mradi wa mchezo "Kuokoa Penguini," amba oni mchezo shirikishi ulioundwa kufundisha wachezaji juu ya mabadiliko ya tabianchi na suluhu zake.

Astrid Peraza anafanya kazi kuhusu masuala ya uundaji upya wa ardhi nchini Kosta Rika.
UNCCD
Astrid Peraza anafanya kazi kuhusu masuala ya uundaji upya wa ardhi nchini Kosta Rika.

Pia amekuwa akishiriki kikamilifu katika mradi wa upandaji miti wa mikoko wa Vivero Verde Mar katika nchi hiyo ya Amerika ya Kati, ambao unasaidia uhifadhi wa mazingira na ambao unasaidia kuzuia kuenea kwa jangwa katika maeneo ya pwani.

"Kuja pamoja ni muhimu sana ili kuondokana na ugumu wa kuenea kwa jangwa katika jamii," amesema na kuongeza kuwa "kwa sababu tunapozungumza juu ya mabadiliko ya tabianchi kufanya kazi peke yake sio chaguo."









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/story/2024/12/1182801

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy