Content-Length: 107162 | pFad | http://news.un.org/sw/story/2024/12/1182826

Wanawake wakimbizi kambini Kyangwali Uganda walia kwa ukatili wa majumbani | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wakimbizi kambini Kyangwali Uganda walia kwa ukatili wa majumbani

Kikao cha upatanishi wa mzozo wa nyumbani kwenye ofisi yakongozi wa wakimbizi kyangwali nchini Uganda.
UN News
Kikao cha upatanishi wa mzozo wa nyumbani kwenye ofisi yakongozi wa wakimbizi kyangwali nchini Uganda.

Wanawake wakimbizi kambini Kyangwali Uganda walia kwa ukatili wa majumbani

Wanawake

Siku 16 za uanaharakati wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake zikiendelea kote dunianiwadau mbalimbali katika makaazi ya wakimbizi ya Kyangwlai nchini Uganda pia wanakabiliana na changamoto hiyo ya ukatili dhidi ya wanawake ikiwa ni moja ya cangamoto iliyokita mizizi katika maenedeleo na utulivu kwenye familia na jamii ya wakimbizi kwa ujumla.

Viongozi wa wakimbizi kwa ushirikiano na wadau wengine kama shirika lisilo la kiserikali la Alight Uganda, Ofisi ya Waziri Mkuu na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wamelivalia njuga suala la upatanishi wa mizozo ya majumbani pamoja na uhamasishaji wa kuipuka licha ya changamoto za kifedha ambazo zinaonekana kuwa chachu kubwa ya mizozo hiyo.

Bwana Walter Otim Oyuki, Mwenyekiti wa chama cha wakimbizi ambaye pia ni mkimbizi kutoka Sudan Kusini anayeishi nchini Uganda.
UN News
Bwana Walter Otim Oyuki, Mwenyekiti wa chama cha wakimbizi ambaye pia ni mkimbizi kutoka Sudan Kusini anayeishi nchini Uganda.

Bwana, Walter Otim Oyuk, Mweneykiti wa wakimbizi ameiabia idhaa hii ya Kiswahili kuwa, wanafanya viakao viwili kila wiki ambapo angalau kesi tano za ukatili majumbani zinashughulikiwa.

Hata hivyo amesema, kesi zinasajiliwa kila siku.

Uhamasishaji na upaninishi unasaidia

Kama sehemu ya harakati za siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, wameimarisha uhamasishaji na upatanishi.

“Tulikimbia mzozo nyumbani kwetu lakini inatamausha kuona kwamba hapa pia mizozo inatanda. Inakwamisha maendeleo kwa sababu mwanamke anapkumbwa na ukatili, maendeleo yanakwama n ahata watoto hawapati Amani,” asema Bwana Otim.

Kwa maoni yake matumizi ya pombe ni miongoni mwa vitu vinavyochochea ukatili dhidi ya wanawake katika kambi hiyo ya wakimbizi.

“Hii ni changamotokubwa  sana kwa sababu ulipowasili ulinikuta nikiwa katika kikao cha upatanishi wa ukatili majumbani . Kila Jumatatu na Alhamisi tunakuwa na vikao vya upatanishi wamizozo ya majumbani,” amesema.

Bi. Norah Alo, kiongozi wa wanawake wakimbizi katika makaazi ya wakimbizi ya Kyangwali, anasema mizozo mingi inatokana na mapato ya nyumbani hasa mavuno ya kilimo katika familia.

“Unapata kwamba wamefanya kazi pamoja kama familia lakini wanapovuna mavuno yao shambani, mme anataka kuwa na mamlaka kuu ya mapato yote na kutumia visivyo,” asema Alo.

Bi. Norah Alo, kiongozi wa wanawake wakimbizi katika makaazi ya wakimbizi ya Kyangwali.
UN News
Bi. Norah Alo, kiongozi wa wanawake wakimbizi katika makaazi ya wakimbizi ya Kyangwali.

Kwa mtazamo wake kuna uhitaji wa kuhamasisha jamii zaidi kama njia muhimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake.

“Ni tatizo kubwa linalowakumba wanawake hapa katika kambi ya  Kyangwali,”amesema.

Mwa mujibu wake upatanisho umechangia pakubwam kuleta utulivu katika familia.

Masuala ya usawawa kijinsia ni chachu ya migongano

Kwa upande wake Bwana Ibrahim Balume, sababu kuu ya mizozo sasa ni wanaume na wanawake kutojua mipaka ya uhusiano wao katika kampeni ya kuchagiza usawa wa kijinsia.

“Shida ni kwamba wanaume nao wanafanyiwa ukatili lakini wao hawajitokezi kulalamika na hata wakilalamika hawasikilizwi kama ilivyo kwa wanawake. Hicho kinaacha mizozo ikitanda zaidi,” amesema Bwana Balume.

Hafutilii mbali kuwa kupunguzwa kwa mgao wa chakula kwa wakimbizi na changamoto za kifedha kunachochea ukatili dhidi ya wanawake kwani kidogo kilichopo kinazozaniwa.

Balume ameongeza kuwa “Kwetu Congo tulikotoka pengo lilikuwa kubwa kati ya mwanamke na mwanume lakini tulipofika Uganda suala la usawa wa kijinsia likatiliwa mkazo mkubwa lakini wanaume wengi limewashinda kuelewa kuwa ni jambo bora na la maana. Wanawake wengine wamevuka mipaka yao na kuzusha vurugu zaidi majumbani.”

Bwana Simon Serugo, Naibu Kamanda wa makazi ya wakimbizi ya Kyangwali.
UN News
Bwana Simon Serugo, Naibu Kamanda wa makazi ya wakimbizi ya Kyangwali.

Ukatili dhidi ya wanawake kwa wakimbizi hatuwezi kuupuza

Bwana Simon Serugo, Naibu Kamanda wa makazi ya wakimbizi ya Kyangwali anakiri kuwa ukatili dhidi ya wanawake na ukatili wa kijinsia kwa ujumula ni changamoto isiyoweza kupuuzwa katika jamii ya wakimbizi ya Kyangwali.

“Ukatili upo na ni dhahiri. Hata hivyo kuna mashirika mengi ya kiraia yanayotusaidia kuhamasisha jamii kukabiliana na changamoto hiyo na hatimaye kuna ahueni,” amesema Bwan Serugo.

Afisa huyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (OPM) ya Uganda ameonesha uhutaji wa ufadhili zaidi kwao na wadau wao ili kuimarisha kampeni za uhamasishaji wa jamii.

Amesema “Kwa mfamo mimi ninatarajiwa kufanya mikutano 7 ya uhamasiahaji katika mwaka mzima wa kifedha lakini huenda haitoshi. Kwenye mikutano hiyo hua tunawahamasiaha watu kuhusu masuala ya kijinsia pia.”

Soundcloud

Makaazi ya wakimbizi ya Kyangwali ni nyumbani kwa wakimbizi zaidi ya 130,000 wengi wakiwa wamekimbia mzozo wa kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) na Sudan Kusini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi limekuwa likihaha kuendeleza ushirikiano na wadau wote kupunguza ukatili wa kijinsia katika makazi hayo na miongoni mwa wakimbizi wote.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/story/2024/12/1182826

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy