Content-Length: 105040 | pFad | http://news.un.org/sw/story/2024/12/1183206

Pedersen awasili Syria na kusema mchakato wa kisiasa uongozwe na wasyria wenyewe | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pedersen awasili Syria na kusema mchakato wa kisiasa uongozwe na wasyria wenyewe

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Geir O. Pedersen akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili mji mkuu Damascus, 15/12/2024
Tahseen Saour
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Geir O. Pedersen akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili mji mkuu Damascus, 15/12/2024

Pedersen awasili Syria na kusema mchakato wa kisiasa uongozwe na wasyria wenyewe

Amani na Usalama

Mabadiliko tunayoona hivi sasa baada ya kuanguka kwa utawala wa Assad yamekuwa ni makubwa, na bila shaka mabadiliko hayo ni fursa ya matumaini makubwa, lakini sote tunafahamu kuna changamoto nyingi mbele yetu, hivyo lazima tuelewe hilo mapema kabisa, amesema Geir O. Pedersen Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria baada ya kuwasili mji mkuu wa taifa hilo Damascus leo Jumapili.

Amewasili Damascus leo ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayat Tahrir al-Sham, HTS walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi, kutwaa mji huo na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.

Bwana Pedersen amewaambia waandishi wa habari kuwa kutokana na hali ya sasa amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuanzisha haraka mchakato wa kisiasa unaojumuisha wasyria wote. Mchakato ambao amesema uongozwe na wasyria wenyewe, wawajibike wasyria wenyewe kwa usaidizi.

Taasisi za serikali zianze kazi

Kuhakikisha taasisi za kitaifa zinarejeshwa na zinafanya kazi, ni jambo ambalo amesema ni changamoto ambayo hata serikali inayoshikilia mamlaka sasa inatambua. Hilo ni muhimu ili kuendeleza kutoa huduma, kusimamia utawala wa sheria na usalama akisema ni jambo muhimu.

Bwana Pedersen akazungumzia pia janga la kibinadamu linalogubika raia wa Syria akisema tunataji kuhakikisha Syria inapokea msaada wa haraka wa kibinadamu kwa raia wake na wakimbizi wanaotaka kurejea nyumbani. Hii ni muhimu sana.

Tweet URL

Tusaidie ikwamuke kiuchumi

Na bila shaka ni kukwamuka kiuchumi kwa Syria ambapo mjumbe huyo maalum amesema “tunahitaji kurekebisha hili haraka. Bila shaka tutaona vikwazo vinaondolewa haraka, ili tuweze kuunganika pamoja na kujenga upya Syria.

Mjumbe huyo Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria akatamatisha kwa kuzungumzia umuhimu wa wahalifu kuwajibika kwa vitendo vyao akisema, tunahitaji kuona mwelekeo wa haki na uwajibikaji kwa vitendo vya uhalifu. Na tunahitaji kuhakikisha kuwa hilo linafanyika kupitia mfumo halali wa haki na kwamba hakuna visasi.

Vikwazo dhidi ya Syria?

Alipoulizwa kuhusu kuondoa vikwazo dhidi ya Syria Bwana Pedersen amesema “unajua hebu sikiliza, bila shaka vikwazo na nimesema mara kwa mara si vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Ni vikwazo vilivyowekwa na Marekani na Muungano wa Ulaya, na pengine wengine wachache.

Na kama anaunga mkono kuondolewa kwa vikwazo hivyo, Bwana Perdersen amesema “sikiliza, ndio,  nafikiri tunahitaji kama nilivyosema, mchakato sahihi na ninasubiri kwa hamu kuendeleza majadiliano na serikali inayoshikilia mamlaka Syria na mamlaka hapa.”









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/story/2024/12/1183206

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy