Content-Length: 99104 | pFad | http://news.un.org/sw/story/2024/12/1183431

Kipimo cha GeneXpert chaleta mapinduzi kwenye upimaji wa VVU Ghana | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipimo cha GeneXpert chaleta mapinduzi kwenye upimaji wa VVU Ghana

Kipimo cha GeneXpert chaleta mapinduzi kwenye upimaji wa VVU Ghana.
UNICEF
Kipimo cha GeneXpert chaleta mapinduzi kwenye upimaji wa VVU Ghana.

Kipimo cha GeneXpert chaleta mapinduzi kwenye upimaji wa VVU Ghana

Afya

Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua. 

Video ya UNICEF Ghana inaanza na simulizi ya mama huyu jina lake limehifadhiwa. Yeye anaishi na Virusi Vya Ukimwi.

Anasema .. nina watoto watano, mmoja wa kike na wanne ni wa kiume. Wakati wa ujauzito wahudumu wa afya waliniambia kuwa mtoto wangu atapata dawa husika akishazaliwa. Alipozaliwa nilimpatia mwanangu dawa kwa wiki sita.

Baada ya hapo mtoto akafanyika vipimo vya VVU na mama aliambiwa majibu yatatoka ndani ya mwezi mmoja. Lakini haikuwa hivyo. Ilipita miezi kadhaa bila taarifa yoyote.

Anasema nilianza kuingia hofu na wasiwasi kwa sababu nilitaka kufahamu hali ya kiafya ya mtoto wangu. Hatimaye baada ya kusubiri kwa miezi minne majibu yalitoka na hakuwa na VVU.

Ili kuondoa vikwazo vya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030, UNICEF na wadau wakapatia Wizara ya Afya ya Ghana kipimo cha uchunguzi wa VVU kiitwacho GeneXpert. Kipimo kilipelekwa katika wilaya tano za mashariki mwa Ghana ambazo ni Suhum, Lower Manya, Kwahu Magharibi, Asuogyaman na Nsawam Adoyagyiri. Paul Dsane – Aidoo ni  mtaalamu wa afya.

« Kipimo cha GeneXpert kwa ajili ya kupima VVU mapema kwa watoto wachanga  kimeonesha kwamba baada ya kusubiri siku 90 kupata majibu ya watoto, sasa ni hadi saa 48. Hii ina maana matibabu kwa watoto yanaweza kuanzishwa mapema. Kipimo hiki kinatumika pia kupima kiwango cha VVU kwenye damu ya mama. Na kwa wajawazito walio na maambukizi ya VVU inaweza kushughulikiwa kabla hajajifungua na hii inaokoa maisha ya mtoto asiambukizwe VVU. »

Kwa mama huyu kipimo hiki kimeleta mabadiliko kwani anasema niliweza kupokea majibu ya mtoto wangu wa mwisho ndani ya siku chache.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://news.un.org/sw/story/2024/12/1183431

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy