Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno Akraba
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno “AKRABA.”
19 DESEMBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Syria, ambako viongozi wa ngazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa wamendelea kusisitiza hitaji la kutanguliza ulinzi wa manusura na uhifadhi wa ushahidi wa uhalifu. Pia tunapata ufafanuzi wa neno na muhtasari wa habari.
FAO Tanzania yatoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa wenyeji Tanzania kupitia Mradi wa ACP MEAs 3
Mradi wa ACP MEAs 3 unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, na kufadhiliwa na Muungano wa Ulaya, EU umetoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wakulima nchini Tanzania. Mradi huu unawapa wakulima zana na ujuzi muhimu katika ufugaji nyuki endelevu, na hivyo kuboresha maisha yao huku wakikuza bayoanuwai na uhifadhi wa mazingira. Kwa kuunga mkono jamii za wenyeji, Mradi huu unalenga kukuza ukuaji wa uchumi na kuwawezesha wakulima kulinda wachavushaji, ambao ni muhimu kwa uzalishaji katika kilimo na afya ya mfumo ikolojia.
Harakati za wazazi kuona watoto wao wanasajiliwa nchini mwao baada ya kuzaliwa
Tarehe 11 mwezi huu wa Desemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilitoa ripoti yake kuhusu usajili wa vizazi duniani ikionesha maendeleo makubwa katika idadi ya watoto wanaosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Maeneo mengine kama nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ongezeko ni dogo ikilinganishwa na kwingineko. Ingawa hivyo licha ya changamoto zilizoko kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara katika kutoa huduma hiyo, mafanikio yanaanza kuonekana kama inavyosimulia makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi kupitia video ya UNICEF.
Sasa tunalima mboga shuleni na nyumbani - Wanafunzi Buhigwe Tanzania
Kupitia mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP, awamu ya Pili, Shule ya Msingi Buhigwe, iliyoko wilayani Buhigwe, mkoa wa Kigoma, ilipatiwa mafunzo kupitia Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), likishirikiana na asasi isiyo ya kiserikali RECODA. Mafunzo haya yalilenga mbinu bora za kilimo ambapo wanafunzi waliweza kuanzisha bustani za mboga kupitia somo la Elimu ya Kujitegemea. Mradi umeanza kutekelezwa na matunda yanaanza kuonekana kama asimuliavyo Assumpta Massoi kwenye makala hii.