Namayombo Mgonela: Utamaduni wa Kiswahili umeniinua kiuchumi
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na kuzungumza na Namayombo Nyanzala Mgonela, mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vilivyoko Karibea St.