Content-Length: 91104 | pFad | https://news.un.org/sw/focus/syria

SYRIA | | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SYRIA

Syria

Damascus, mji mkuu wa Syria
UN News/Nabil Midani

“Mustakabali wa Syria ni suala lao kuamua, na Mjumbe wangu Maalum atakuwa akifanya kazi nao kwa lengo hilo. Narudia wito wangu wa utulivu na kuepuka ghasia wakati huu nyeti, huku haki za wasyria wote zikilishwa bila ubaguzi.

António Guterres, Katibu Mkuu wa UN 08 Desemba 2024

SYRIA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema baada ya miaka 14 ya vita vya kikatili na kuanguka kwa utawala wa kidikteta, leo hii watu wa Syria wanaweza kukumbatia fursa ya kihistoria kujenga mustakabali thabiti na wa amani.

Tangu machi 2011, Syria imekuwa katika mgogoro ambao umewalazimisha watu zaidi ya 500,000 kutoroka makazi yao. Mamilioni ya raia wa Syria sio tu ni wamekimbia nchi yao, bali pia mamilioni wengine wamekuwa wakimbizi wa ndani. Mgogoro huu unachukuliwa kuwa mbaya zaidi wa kibinadamu kipindi hiki ambapo watu zaidi ya milioni 13 wanahitaji msaada na unalaumiwa kwa kusababisha wanaume, watoto pamoja na wanawake wengi wa Syria kutaabika.

 

HATUA ZA KIBINADAMU

Watu mamia kwa maelfu wameuawa na mamilioni wamelazimishwa kukimbia tangu Machi 2011, wakati mapigano yalipoanza nchini Syria kati ya serikali na makundi yanayotaka kumuondoa madarakani rais Bashar al- Assad. UN ikiwa na washirika wake inajaribu kutoa mahitaji ya msaada wa kibinadamu.

HABARI ZA UN KUHUSU SYRIA

Bofya hapa kupata habari za Umoja wa Mataifa kuhusu Syria.

 

MJUMBE MAALUM KUHUSU SYRIA

Mwezi Januari mwaka 2019, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alimteua Geir O. Pedersen kuwa mjumbe wake maalum wa 4 kwa Syria. Hivi sasa anaongoza jitihada za UN za kusongesha utekelezaji wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2254 la mwaka 2015  na pia tamko la pamoja la Geneva la mwaka 2012. Bwana Pedersen anafanya kila juhudi kuweza kuleta kwenye meza ya mazungumzo , makundi yote yanayohusika ili kuweza kumaliza vita. mazungumzo yanazingatia azimio hilo namba 2254 yakimulika  utawala, ratiba na mchakato wa kupanga katiba mpya na kufanyika uchaguzi mkuu kama msingi wa mchakato wa Syria wa kumaliza mgogoro huo. Pia mazungumzo yanahusu mikakati dhidi ya ugaidi.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://news.un.org/sw/focus/syria

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy