Content-Length: 103428 | pFad | https://news.un.org/sw/story/2024/12/1183006

Syria iko njiapanda ikiwa na hatari lakini fursa ya kubadili mustakbali: UN | Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria iko njiapanda ikiwa na hatari lakini fursa ya kubadili mustakbali: UN

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Geir Pedersen akihutubia waandishi wa habari mjini Geneva kuhusu mashauriano kuhusu katiba mpya ya Syria
UN Photo
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Geir Pedersen akihutubia waandishi wa habari mjini Geneva kuhusu mashauriano kuhusu katiba mpya ya Syria

Syria iko njiapanda ikiwa na hatari lakini fursa ya kubadili mustakbali: UN

Amani na Usalama

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Geir Pedersen, amesema hakuna kinachopaswa kuzuia uhamishaji wa amani wa Madaraka nchini Syria kufuatia kuenguliwa ikwa utawala wa Rais Bashar- Al Assad.

Akizungumza hii leo na waandishi wa habari Pedersen amesema baada ya mkutano wa kikosi kazi cha masuala ya kibinadamu huko Geneva “Syria sasa iko katika njia panda yenye fursa kubwa kwetu, lakini pia ina hatari kubwa. Na tunahitaji kuziangalia vyote viwili. "

Ameongeza kuwa “Tunajua kwamba, bila shaka, HTS sasa ni kundi kubwa katika udhibiti wa Damascus, lakini ni muhimu pia kukumbuka kwamba sio kundi pekee lenye silaha huko Damascus."

Huku kukiwa na picha za matukio ya shangwe katika mitaa ya Damascus kufuatia mwisho wa utawala wa Assad, Bwana Pedersen ametahadharisha kwamba uhamishaji wa mamlaka umeambatana na ripoti za wizi na uvamizi wa majengo ya umma au nyumba za watu binafsi.

“Lakini hii inaonekana imekoma na hilo ni jambo zuri,” aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva.

Mhudumu wa dharura wa kwanza anakimbia baada ya mashambulizi ya makombora yaliyolenga hospitali na kambi za watu waliokimbia makazi yao huko Idleb, Syria.
© UNOCHA/Ali Haj Suleiman
Mhudumu wa dharura wa kwanza anakimbia baada ya mashambulizi ya makombora yaliyolenga hospitali na kambi za watu waliokimbia makazi yao huko Idleb, Syria.

Mashambulizi mila ya Golan lazima yakome

Akigeukia ripoti nyingi kuhusu harakati za wanajeshi wa Israel katika milima ya Golan inayokaliwa na mashambulizi ya mabomu ya kulenga shabaha ndani ya Syria, Bwana. Pedersen amesisitiza kwamba "Hili linahitaji kukomeshwa. Sina mawasiliano na Waisraeli, lakini bila shaka, Umoja wa Mataifa huko New York wanawasilina nao. Na, unajua, walinda amani walioko milima ya Golan, wanawasiliana kila siku na Waisraeli. Na pasi shaka, ujumbe kutoka New York ni sawa tu kwamba kile tunachokiona ni ukiukaji wa makubaliano ya 1974 ya kujiengua kutoka eneo hilo”.

Hadhi ya HTS kuwa magaidi huenda ikabadilika

Bwana Pedersen amesema hadhi ya HTS kuwa katika orodha ya kundi la kigaidi huenda ikabadilika akifafanua kuwa "Lazima uangalie ukweli na kuona kile ambacho kimetokea katika miaka tisa iliyopita. Ni miaka tisa tangu azimio hilo lilipopitishwa na ukweli uliopo hadi sasa ni kwamba HTS na pia makundi mengine yenye silaha yamekuwa yakituma ujumbe mzuri kwa watu wa Syria, wamekuwa wakituma jumbe za umoja, ushirikishwaji na kusema kwa uwazi, pia tumeshuhudia huko Aleppo na Hama, pia tumeona, wakiahidi mambo kuwa shwari.”

Naye B.i Najat Rochdi, Naibu Mjumbe Maalumu wa wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria, ameitisha mkutano na kikosi kazi cha masuala ya kibinadamu huko Geneva akiwataka wadau na nchi wanachama wenye uwezo kuweka kipaumbele cha ulinzi wa raia, kulinda miundombinu muhimu, na kuhakikisha kuwa taasisi za Syria zinaendelea kufanya kazi ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa.

Ameongeza kuwa “Matukio yanayoendelea kwa kasi nchini Syria yanaleta mahitaji mapya juu ya yale ambayo yalikuwepo awali ikiwemo wimbi jipya la wakimbizi wa ndani linalosababishwa na migogoro, wakimbizi wanaorejea kwa makundi kutoka nchi jirani, na maelfu ya wafungwa walioachiliwa hivi karibuni wanaohitaji msaada wa haraka , ikiwa ni pamoja na makazi na usafiri.”

Bi Rochdi amesisitiza zaidi haja ya kuongezwa ulinzi na uwezo wa ufuatiliaji, na kutoa wito kwa nchi wanachama wenye uwezo wa kuhakikisha raia wanaokimbia mapigano wanapita salama.

Pia mesema Miundombinu muhimu, ikijumuisha shule na vituo vya huduma ya afya, lazima ihifadhiwe, na njia za raia kukimbia ghasia kwa usalama au kurudi nyumbani, inapowezekana, lazima zibaki wazi.

Msichana aliyekimbia vurugu zinazozidi kuongezeka huko Aleppo na familia yake akiwasili katika kituo cha mapokezi katika mji wa Ar-Raqqa, Syria.
© UNICEF/Muhannad Aldhaher
Msichana aliyekimbia vurugu zinazozidi kuongezeka huko Aleppo na familia yake akiwasili katika kituo cha mapokezi katika mji wa Ar-Raqqa, Syria.

Misaada muhinu lazima iendelee kwa raia

Mratibu wamisaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ofisi ya kuratibu misaada hiyo OCHA Tom Fletcher kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter amesema mambo mengi bado yako njia panda Syria lakini msaada muhimu unaohitajika kwa raia lazima uendelee kutolewa.

Amesema “masuala kama huduma za msingi za afya na huduma zinginhe za kibinadamu lazima ziendelee kuwepo.”

Bwana Fletcher amesisitiza kwamba wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wtaendelea kutsaidia kwa kila njia pale inapowezekana ili kusaidia raia wa Syria.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba “Kuna fursa kubwa kwa Syria kuelekea kwenye amani na watu wake kuanza kurejea nyumbani. Lakini hali bado haijulikani”.

Limeongeza kuwa “Na kutokana na miundo mbinu iliyovurugika na asilimia 90 ya watu wakitegemea misaada ya kibinadamu, msaada wa haraka unahitajika ili kukidhi mahitaji ya msingi ya maelfu ya watu walioathirika na machafuko.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://news.un.org/sw/story/2024/12/1183006

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy